Project Canterbury

Kitabu Cha Sala Wa Watu Wote
The Book of Common Prayer in Swahili

London: SPCK, 1906.


JINSI INAVYOPASA KUZISOMA ZABURI.

ZABURI zote zisomwe marra moja killa mwezi, kama ilivyoamriwa kule, wakati wa Sala za Assubuhi na Jioni. Lakini mwezi wa February zisomwe mpaka siku ya ishirini na nane au ishirini na kenda tu.

Na miezi January, March, May, July, August, October na December, ina siku thelathini na moja; bassi imeamriwa, Zaburi zile zile zisomwe siku ya mwisho ya miezi hiyo, zilizosomwa siku iliyo kabla yake: Zaburi zipate kuanzwa tena siku ya kwanza ya mwezi ufuatao.

Na Zaburi ya mia na tissatashara imegawanywa kua sehemu ishirini na mbili, na sehemy hizi ni nyingi, haziwezi kusomwa wakati mmoja; bassi kwa wakati mmoja zimeamriwa sehemu nne, au tano.

Na mwisho wa killa Zaburi, na wa killa sehemu ya Zaburi ya mia na tissatashara, usemwe Uimbo huu,

Utukufu una Baba, na Mwana: na Roho Mtakatifu;
Ulivyokuwa mwanzo: ulivyo sasa, utakavyokuwa milele. Amin.

Zaburi zimetengenezwa kama zilivyoandikwa kwa Kiebrania.

Fahamu tena, wakati wo wote atakapopenda askofu, ni halali, kwa khiari yake, kutia zaburi nyingine badale ya zile zilizoamriwa katika kitabu cha Zaburi.


Project Canterbury