Swali. Jina lako nani?
Jibu. [Taja Jina lako la Ubatizo.]
Swali. Nani waliokupa jina hili?
Jibu. Wadhamini wangu katika Ubatizo wangu; nilipofanywa kiungo cha Kristo, mtoto wa Mungu, na mrithi Ufalme wa mbingu.
Swali. Wadhamini wako walikufanyiaje wakati ule?
Jibu. Waliahidi wakaweka nadhiri ya mambo matatu mahali pangu. La kwanza, kwamba nitamkataa Shetani na kazi zake zote, mapendezo na naambo yasiyofaa ya dvmia hii mbaya, na tamaa mbaya zote za mwili. La pili, kwamba nitaziamini sharti zote za Imani ya Kikristo. Na la tatu, kwamba nitayashika mapenzi na amri takatifu za Mungu, na kuzifuata siku zote za maisha yangu.
Swali. Huoni bassi ya kwamba imekupasa kuamini na kufanya kama walivyoahidi kwa ajili yako?
Jibu. Kweli, naona; na kwa msaada wa Mungu nitafanya. Nami namshukuru kwa moyo Baba yetu wa mbinguni, kwa maana ameniita nipate hali hii ya wokofu, kwa Yesu Kristo Mwokozi wetu. Tena namwomba Mungu anipe neema yake, nipate kudumu katika hali hiyo hatta mwisho wa maisha yangu.
Mwalimu. Sema Sharti za Imani yako.
Jibu. Narnwamini Mungu Baba Mwenyiezi, Muumba mbingu na inchi:
Na Yesu Kristo Mwana wake pekee, Bwana wetu, Aliyechukuliwa mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu, Akazaliwa na Bikira Mariamu, Akateswa zamani za Pontio Pilato, Akasulibiwa, Akafa, Akazikwa, Akashuka mahali pa wafu; Siku ya tatu akafufuka, Akapaa mbinguni, Anaketi mkono wa kuume Ava Mungu Baba Mwenyiezi, Kutoka huko atakuja kuwahukumu watu wahayi na wafu.
Namwamini Roho Mtakatifu; Kanisa Takatifu, Katholiko; Ushirika wa Watakatifu; Ondoleo la dhambi; Kiyama ya mwili; Na uzima wa milele. Amin.
Swali. Mambo gani makuu unayofundishwa katika sharti hizi za Imani yako?
Jibu. Kwanza, nafundishwa kumwamini Mungu Baba, aliyeniumba mimi, na ulimwengu wote.
La pili, kumwamini Mungu Mwana, aliyenikomboa mimi, na wana Adamu wote.
La tatu, kumwamini Mungu Roho Mtakatifu, anitakasae mimi, na watu wateule wa Mungu wote.
Swali. Ulisema, ya kwamba Wadhamini wako waliahidi mahali pako, kwamba utazishika Amri za Mungu. Niambie, kuna amri ngapi?
Jibu. Kumi.
Swali. Amri zipi hizo?
Jibu. Zile alizozinena Mungu katika sura ya ishirini ya Kitabu cha Kutoka, akisema, Mimi nclimi Bwana Mungu wako, niliyekutoa katika inchi ya Misri, katika nyumba ya ntumwa.
I. Usiwe na miungu wengine illa mimi.
II. Usijifanyizie sanamu ya kuchora, wala mfano wa kitu cho chote kilichoko juu mbinguni, wala chini duniani, wala majini chini ya inchi. Usivisujudu, usiviabudu: kwani mimi Bwana Mungu wako Mungu mwivu, nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hatta kizazi cha tatu na cha nne chao wanichukiao; nami nawarehemu elfu elfu wanipendao, na kushika amri zangu.
III. Usilitaje burre Jina la Bwana Mungu wako, kwani Bwana hatamtoa khatiyani alitajae Jina lake burre.
IV. Ikumbuke siku ya Sabato, itakase. Siku sita fanya kazi, tenda mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana Mungu wako; Usitende kazi yo yote, wevve, wala mwanawo, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala nyama zako, wala mgeni aliomo nyumbani mwako. Kwani kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na inchi, bahari na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba: kwa sababu hii Bwana akaibariki siku ya saba akaitakasa.
V. Waheshimu baba yako, na mama yako; siku zako zipate kuzidi katika inchi upewayo ria Bwana Mungu wako.
VI. Usiue.
VII. Usizini.
VIII. Usiibe.
IX. Usimshuhudie jirani yako uwongo.
X. Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ngombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.
Swali. Mambo gani makuu unayofundishwa katika amri hizo?
Jibu. Naf undishwa mambo mawili: yanipasayo kwa Mungu, na yanipasayo kwa Jirani yangu.
Swali. Imekupasaje kwa Mungu?
Jibu. Imenipasa kwa Mungu, kumwamini, kumcha, na kumpenda, kwa moyo wangu wote, kwa akili zangu zote, kwa roho yangu yote, na kwa nguvu zangu zote; kumwabudu, kumshukuru, kumtumainia kabisa, kumwomba, kuliheshimu Jina lake takatifu na Neno lake, na kumtumikia vema siku zote za maisha yangu.
Swali. Imekupasaje kwa Jirani yako?
Jibu. Imenipasa kwa Jirani yangu, kumpenda kama nafsi yangu, na kuwatendea watu wote, kama nitakavyo wao wanitendee mimi: Kuwapenda, kuwaheshimu, kuwasaidia baba na mama yangu: Kumheshimu na kumtii Mfalme, na wakuu wote walio chini yake: Kujitiisha kwa wakubwa wangu, waalimu wangu, mapadri na bwana zangu: Kunyenyekea mbele zao wote walio wakubwa kuliko mimi: Kujiangalia nisimdhuru mtu kwa neno wala kwa tendo: Kuwa adili na mwenye haki katika shughuli zangu zote: Kutokuwa na kinyongo wala machukio moyoni mwangu: Kuizuia mikono yangu isiibe kitu cho chote, ulimi wangu usitukane, wala usiseme uwongo, wala usisingizie: Kujiangalia mwili wangu niwe na kiasi, nisiwe mlevi, wala asharati: Nisitamani wala kutaka mali ya watu; lakini kujifunza na kufanya kwa bidii kazi ya kunipatia riziki zangu, na kutenda yanipasayo katlka hali, Mungu atakayopenda kuniitia.
Mwalimu.
Mwanangu, fahamu ya kwamba huwezi kuyatenda mambo haya kwa nguvu zako, wala kuzif uata Amri za Mungu, wala kumtumikia, usipokuwa na neema yake; bassi huna buddi kujifunza kutaka daima neema hiyo kwa kuomba sana. Nataka nikusikie, bassi, kama waweza kusema Sala ya Bwana.
Swali. Baba yetu, uliye mbinguni, Jina lako liwe takatifu. Ufalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe duniani, Kama yatimizwavyo mbinguni. Utupe leo riziki zetu. Utusamehe makosa yetu, Kama sisi tunavyowasamehe waliotukosa. Usitutie majaribuni; Lakini utuokoe maovuni. Amin.
Swali. Ni nini utakayo kwa Mungu katika Sala hii?
Jibu. Namtaka Bwana Mungu wangu, Baba yetu wa mbinguni, mtoa wema wote, anipelekee mimi na watu wote neema yake; tupate kumwabudu, kumtumikia, na kumtii, kama itupasavyo. Namwomba tena Mungu atupelekee riziki zetu zote za roho na za mwili; aturehemu, atusamehe dbambi zetu; apende kutuokoa na kutuhifadhi na khatari zote za roho na za mwili; atulinde na dhambi na maovu yote, na adui wetu wa robo, na mauti ya milele. Na hayo natumaini kuwa atayafanya kwa rehema zake na wema wake, kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Kwa sababu bii nasema, Amin, Yafanyike.
Swali. Kuna Sakramenti ngapi alizoamuru Kristo katika Kanisa lake?
Jibu. Mbili tu, zilizo faradbi kwa wokofu wa watu wote, nazo ni Ubatizo, na Chakula cha Bwana.
Swali. Neno hili Sakramenti maana yake nini?
Jibu. Sakramenti ni dalili ya nje, na inayoonekana kwa macho, ya neema ya ndani na ya rohoni tunayopewa, imeamriwa na Kristo mwenyewe, kuwa njia ya kupokelea neema biyo, na kuwa arabuni ya kutuyakinisha.
Swali. Kuna sehemu ngapi katika Sakramenti?
Jibu. Mbili; dalili ya nje na inayoonekana, na ueema ya ndani na ya rohoni.
Swali. Dalili ya nje na inayoonekana kwa macho katika Ubatizo ni nini?
Jibu. Ni maji; mtu abatizwayo kwayo Kwa Jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.
Swali. Neema ya ndani na ya rohoni ni nini?
Jibu. Kufa kwa mambo ya dhambi, na kuzaliwa marra ya pili katika haki; Kwani tukiwa kwa asili tumezaliwa dhambini, na watoto wa ghadhabu, kwa Ubatizo tumefanyika watoto wa neema.
Swali. Watu watakaobatizwa wamepasiwa nini?
Jibu. Toba, illi waache dhambi; na Imani, illi waziamini sana ahadi za Mungu walizopewa katika Sakramenti hii.
Swali. Kwani, bassi, huwabatiza watoto Avachanga, nao wakiwa hawawezi kutenda haya kwa kuwa wadogo?
Jibu. Kwa sababu wanaahidi mambo haya yote mawili kwa vinywa vya Wadhamini wao; na wakipata kuwa watu wazima imewapasa wenyewe waifikilize ahadi hiyo.
Swali. Kwa kusudi gani Sakramenti ya Chakula cha Bwana irueamriwa?
Jibu. Kuwa kumbukumbu la siku zote la dhabihu ya kufa kwake Kristo, na la mambo mema tunayopokea kwa kumbukumbu hilo.
Swali. Nini sehemu ya nje au dalili ya nje katika Ohakula cha Bwana?
Jibu. Mkate na Divai, alivyoamuru Bwana vipokewe.
Swali. Nini sehemu ya ndani, au kitu kinachoashiriwa?
Jibu. Mwili na Damu ya Kristo zinazotwaliwa na kupokewa kwa kweli na pasipo shaka na waamini katika Ohakula cha Bwana.
Swali. Mambo gani mema tupatayo kwa Mwili na Damu ya Kristo?
Jibu. Kwa Mwili na Damu ya Kristo twapata nguvu na kuburudishwa roho zetu, kama vile miili yetu inavyopata nguvu na kuburudishwa kwa mkate na divai.
Swali. Wale wajiao Ohakula cha Bwana wamepasiwa nini?
Jibu. Kujihoji, kama kweli wametubia dhambi zao za zamani, na kukusudia sana kuishi rnaisha mapya; na kama wanaziamini sana rehema za Mungu zilizo katika Kristo, na kukumbuka kwa shukrani kufa kwake; na kama wana upendano na watu wote.
¶ Watoto wakiisha kupata umri wa kufaa, nao waweza kusema na kufahamu Imani, Sala ya Bwana, na Amri Kumi, na kujibu maswali ya Katekisimo hii fupi; waletwe kiva Askofu. Na killa mtoto awe na Mdhamini, mivcmamume au mwanamke awe shahidi wa Kupewa Kipa Imara kwake.
¶ Askofu, aagizapo watoto waletwe kwake illi wapewe Kipa Imara, Mchungaji wa killa mtaa alete au apeleke karatasi yenye sahihi ya mkono wake, na inajina ya watoto wote wa mtaa wake, awaonao wa tayari kupewa Kipa Imara. Na, Askofu akiwakubali, aweke mikono yake juu ya vichwa vyao, kama ifuatavyo.
Project Canterbury