KUTUMIKA WAKATI WA SALA YA ASSUBUHI. ¶ Ungamo hili la Imani yetu linalokwitwa na watu Imani ya Athanasio Mtakatifu liimbwe au lisemwe na Mkhudumu na watu Siku ya Kuzaliwa Kristo, Epifania, siku ya Mattiya Mt., Pasaka, Siku ya Kupaa Kristo, Pentekote, na siku za Yohana Mbatizaji, Yakobo, Bartolomayo, Mattayo, Simon na Yuda, Andrea, na Juma a pili ya Utatu, wakati wa Sala ya Assubuhi badala ya Imani ya Mitume; na watu wote wasimame.
QUICUNQUE VULT. Killa atakae kuokoka: zaidi ya yote imemlazimu kuishika Imani Katholiko.
Nayo asipoilinda pasipo kuipunguza wala kuiharibu: bila shaka atapotea milele.
Na Imani Katholiko ni hii: tumwabudu Mungu minoja katika Utatu, na Utatu katika Umoja;
Tusizichanganye nafsi: wala kuigawanya asili.
Kwa maana nafsi ya Baba mbali, nafsi ya Mwana mbali: nafsi ya Koho Mtakatifu mbali.
Bali Uungu wa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu ni Uungu umoja: Uttikufu wao sawa, Ukuu wao wa milele.
Kama alivyo Baba, ndivyo alivyo Mwana: ndivyo alivyo Roho Mtakatifu.
Baba hakuumbwa, Mwana hakuumbwa: Roho Mtakatifu hakuumbwa.
Baba hana mpaka, Mwana hana mpaka: Roho Mtakatifu hana mpaka.
Baba wa milele, Mwana wa milele: Roho Mtakatifu wa niilele.
Walakini hakuna watatu walio wa milele: illa Mmoja aliye wa milele.
Kadhalika hakuna wata'tu wasioumbwa, wala watatu wasio na mpaka: illa mmoja tu asiyeumbwa, na mmoja tu asiye na mpaka.
Kadhalika Babani Mwenyiezi, Mwana ni Mwenyiezi: na Roho Mtakatifu ni Mwenyiezi.
Bali hakuna Watatu walio Wenyiezi: illa aliye Mwenyiezi ni mmoja tu.
Yivyo hivyo Baba ni Mungu, na Mwana ni Mungu: na Roho Mtakatif u ni Mungu.
Bali hakuna Miunguwatatu: illa Mungu mmoja tu.
Vivyo bivyo Baba ni Bwana, na Mwana ni Bwana: na Roho Mtakatifu ni Bwana.
Bali hakima Bwanawatatu: illa Bwana mmoja tu.
Kwa maana kama tunavyoshurutishwa kwa kanuni ya kweli ya Kikristo: kukiri ya kuwa killa nafsi ni Mungu na Bwana;
Kadbalika tunagombezwa na Imani Katholiko: tusiseme ya kuwa wako Miungu watatu au Bwana watatu.
Baba hakuumbwa na aliye yote: wala hakukhulukiwa wala hakuzaliwa.
Mwana anatoka katika Baba tu: bakuumbwa, wala hakukhulukiwa, bali anazaliwa.
Roho Mtakatifu anatoka katika Baba na katika Mwana: hakuumbwa,wala hakukhulukiwa, wala hakuzaliwa, bali anatoka.
Bassi yupo Baba mmoja tu, si Baba watatu; yupo Mwana mmoja tu, si Wana watatu: yupo Roho Mtakatifu mmoja tu, si Roho Watakatifu watatu.
Na katika Utatu huu hapana aliye wa kwanza na aliye wa baadae: hapana aliye mkuu zaidi na aliye mdogo.
Bali nafsi zote tatu ni wa milele: wa sawa wote.
Bassi katika mambo yote kama tulivyokwisha kusema: imetulazimu kuuabudu Umoja katika Utatu, na Utatu katika Umoja.
Bassi yeye atakae kuokoka: audhanie hivi Utatu.
Na zaidi ya haya, apate wokofu: imemlazimu kukuamini kwa moyo Kufanyika mwili kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
Na Imani kamili ndiyo hii: tuamini, tukiri ya kuwa Bwaiia wetu Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, ni Mungu na Mwana Adamu.
Ni Mungu, ana asili ya Baba, amezaliwa kabla ya zamani zote: ni Mwana Adamu, ana asili ya Mama wake, alizaliwa katika zamani.
Mungu kamili na Mwana Adamu kamili: ana roho yenye akili na mwili wa Mwana Adamu.
Yu sawa na Baba kwa kuwa ni Mungu: Yu chini ya Baba kwa kuwa ni Mwana Adamu.
Na ijapokuwa yu Mungu na Mwana Adamu: yeye si wawili illa Kristo mmoja.
Yeye ni mmoja, si kana kwamba Uungu urnebadilika uwe mwili: bali kwa kuitwaa asili ya Mwana Adamu na kuiunga na Uungu.
Mmoja kabisa; si kwa kuzichanganya asili zile mbili: bali kwa kuwa Nafsi mmoja tu.
Kwa maana karaa roho yenye akili pamoja na mwili huwa Mwana Adamu mmoja: kadhalika Mungu na Mwana Adamu pamoja ni Kristo mmoja;
Aliyeteswa kwa wokofu wetu: akashuka mahali pa wafu, akafufuka siku ya tatu.
Akapaa mbinguni, anaketi mkono wa kuume wa Mungu Baba Mwenyiezi: kutoka huko atakuja kuwahukumu watu wahayi na wafu.
Atakapokuja yeye, wana Adamu wote watafufuka na miili yao: watatoa khabari za matendo yao.
Nao waliotenda mema wataingia katika uzima wa milele: nao waliotenda mabaya katika moto wa milele.
Hii ndiyo Imani Katholiko: killa mtu asiyeikubali kwa moyo hawezi kuokoka.
Utukufu una Baba, na Mwana: na Koho Mtakatifu;
Ulivyokuwa mwanzo: ulivyo sasa, utakavyokuwa milele. Amin.
Project Canterbury