Project Canterbury

   

KATEKISIMO FUPI.

MAFUNDISHO

KWA

MAULIZO NA MAJIBU.

 

SO
LI
DEO
GL
OR
IA

ZANZIBAR.

1876.

  


PRINTED AT THE UNIVERSITIES' MISSION PRESS, ZANZIBAR.


I.

Nani aliyekuumba?
Muungu.

Yuko wapi Muungu?
Mahali pote, mbingu na inchi zimejaa naye.

Muungu ni nini?
Ni Roho.

Muungu alikuwa na mwanzo?
Siyo kabisa.

Ni miungu mingapi?
Muungu ni nimoja tu.

Katika Muungu inayo nafai moja tu?
Zinazo nafsi tatu.

Nafsi hizo, ndizo zipi?
Muungu Bab, Muungu Mwana, na Muungu Roho Mtakatifu.

Muungu Mwana na Muungu Roho Mtakatifu walikuwa na mwanzo?
Siyo, walikuwa tangu milele pamoja na Muungu Baba.

Ni hawa miungu mitatu?
Siyo, nafsi tatu, lakini Muungu mmoja kabisa.

Muungu aona na ajua vitu vyote?
Ndio, ajua mawazo yetu yote pia.

Yee aweza kufanya vite vyote?
Ndio, ni'Mweza killa kitu.

Yee ameviumba vitu vyote?
Ndio, ameviumba pasipo kwanza kitu.

Katika majira gain ameviumba?
Katika siku sita.

Kwa nani ameviuma?
Kwa neno lake.

Neno lake ni nani?
Muungu Mwana.

II.

Nani aliyekukomboa?
Isa Masiya, ndiye Muungu Mwana aliyefanywa mwana adamy kja sababu yetu.

Amekukomboaje?
Ameninunua kwa kufa kwake.

Amekukomboa katika nini?
Katika nguvu ya Shetani.

Isa Masiya ndiye Muungu?
Ndio, ni Muungu hálisi ya Muungu hálisi.

Katika Isa Masiya winazo nafsi ngapi?
Moja, ndiye Muungu Mwana.

Ni asili ngapi katika Isa Masiya?
Mbili, asili ya Muungu, na asili ya mwana adamu.

Kwa ajili gain Muungu Mwana amefanywa mwana adamu?
Atutoe sisi katika thambi ne jehannum.

III.

Alikuwa Bwana wetu Isa Masiya sikuzote mwana adamu?
Siyo.

Tangui lini ni mwana adamu?
Zayidi ya miaka themantashara mia.

Amekuwaje mwana adamu?
Alizaliwa na Maryamu mwanamwali aliobarikiwa.

Kwa nguvu gani?
Alichukuliwa mamba kwa Reho Mtakatifu.

Amekwisha kuwa Muungu?
Siyo, ni Muungu pamoja na mwana adamu.

Atakuwa hivyo siku zote?
Ndiyo, hatta milele.

Katika mambo gani amezaliwa Bwana wetu Isa Masiya?
Katika mambo masikini.

Kwaje?
Amezaliwa katika banda mjini Betlehemu.

Hali gani aliyoipata duniani?
Hali ya taabu na huzuni.

Kwa sababu gani?
Amechukiwa na Shetani na watu wenyi thambi.

Kwa ajili gani amesumbuka vibaya?
Kwa sababu ya thambi zetu.

IV.

Alisumbukaje Bwana wetu Isa Masiya?
Kwa kitisho katika bustani na hari ya damu.

Kwa nini tena?
Walimfanyizia mzaha, wakamtukana.

Kwa nini tena?
Alipigqa, akavikwa taji ya miiba, akachukua msalaba wake.

Kwa nini tena?
Alifungwa msalabani kwa mismari hatta akafa katikati ya wanyang'anyi wawili.

Kwa siku ipi alipokufa?
Juma.

Aliuawa wapi?
Kalvarini, mbele ya mlango wa 'mji Yersalemi.

Kwa ajili gani alikufa?
Kuirithika haki ya Muungu na kuzsetiri thambi zetu.

V.

Alipokwisha kufa Bwana wetu Isa Masiya alikuwaje?
Mwili wake ulizikwa, roho yake ikashuka mahali pa wafu.

Mwili wake ukaharibika?
Haukuharibika.

Alifanyanti tena?
Aliondoka katika kaburi.

Kwa siki ipi?
Juma a pili.

Alifanyi tena?
Akapaa mbinguni.

Alipopaa lini?
Siku arobaini haada ya kufufuka.

Akapaa kwa siku ipi?
Alhamisi.

Yuko wapi sasa?
Anakaa mkono wa kuume wa Muungu.

Muungu hana mkono, mkono wake wa kuume nini?
Ndio kwa mfano mahali pa heshima kulikko yote.

VI.

Atakaa sikuzote mkono wa kuume wa Muungu?
Siyo, atarudi.

Atarudi lini?
Kwa siky ya mwisho.

Atakaporudi atafanyani?
Atawaamua walimwengu.

Atatuamuaje?
Kwa vitendo tulivyovifanya katika mwili.

Atatuamua kwa vitendo tu?
Kwa vitendo vyetu, maneno yetu na mawazo yetu yote pia.

Atakujaje?
Kwa nguvu na utukufu mkuu.

Atawaambiani watu wabaya?
Enendeni enyi 'mmelaaniwa, motoni mwa milele.

Atawaambiani watu wema?
Njooni, enyi waliobarikiwa na Baba yangu.

Nani watakaotupeleka barazani kwa hukumu?
Malaika watakatifu.

VII.

Itakapokwisha hukumu, wabaya watapatani?
Watatupwa motoni mwa jehannum, na mwili na robo pamoja.

Watasumbukaje?
Watachomewa na wataumiza milele.

Wenzo wao nani?
Shetani na malika zake.

Shetani nani?
Pepo aliyeanguka mbinguni kwa sababu ya kiburi chake.

Hukumu itakapokwisha, watu wema watapatani?
Wataingia mbinguni pamoja na Masiya.

Mbinguni watapatani?
Watafurahiwa milele na Muungu.

VIII.

Nani ansyekutakasa?
Muungu Roho Mtakatifu.

Anakutakasaje?
Akinifanya mtu mwema na mtakatifu.

Akufanyaje mwema?
Kwa kukaa nami.

Ametoka wapi huyo Roho Mtakatifu?
Ametoka katika Baba na Mwana.

Yee ni sawa na hawa?
Ndio, yee pamoja nao Muungu mmoja na Bwana mmoja.

Amekuja tangu lini kukaa naswi duniani?
Juma ya pili ya Pentekoti.

Anakaa na watu gani?
Anakaa katika Kanisa lo takatifu na lo katoliko.

IX.

Kanisa lo takatifu nini?
Mwili wa Masiya.

Mwili huu nini?
Watu wote wanaoamini wanaambatana kwa kuwa na kitwa kimoja.

Kitwa hiki nani?
Masiya Isa Bwana wetu.

Niambie sifa za Kanisa la Masiya.
Ni moja, ni takatifu, ni Katoliko, ni Apostoliko.

Katoliko - maana yake nini?
Kwa wote, mahali pote, na lenyi kweli yote.

Apostoliko - maana yake nini?
Liliowafuata kwanza Apostoli, ndio mitume wake Masiya, likafuata hatta leo askfau.

Usharika wa watakatifu nini?
Watakatifu wote wanashariki neema ya Muungu na vitu vyema vyote.

Mtu gani ni mtakatifu?
Mtu anayemtumikia kwa moyo Muungu, ao hapa katika inchi, ao huko katika mbingu.

Usharika nini?
Watu wengi wenyi kitu kimoja.

Kanisa la Masiya linayo mafungu mangapi?
Mawili, Kanisa liliokwisha kushinda na Kanisa lifanyalo vita.

Liko wapi Kanisa liliokwisha kushinda?
Mbingumi.

Liko wapi kanisa lifanyalo vita?
Hapa, katika inchi.

Kanisa lifanyalo vita, linalo mafungu mangapi?
Mawili, Padre, ao Wangoje, na watu.

Padre watu gani?
Tume za Muungu.

Zinazo ginsi ngapi za Padre?
Tatu, Asikafu, Kasisi, na Shemasi.

X.

Thambi ndio nini?
Kuivunja sheria ya Muungu.

Zinazo ginsi ngapi za thambi?
Mbili, thambi ya asili na thambi za amali.

Thambi ya asili nini?
Ndio upungufu kwa asili, siswi wote tumezaliwa wenyi thambi hii.

Thambi za amai nini?
Thambi zote tulizozifanya siswi wenyewe.

Thawabu za thambi nini?
Kufa na moto wa Jehannum.

Thambi zinaondokaje?
Kwa sababu ya mateso na mauti ya Bwana wetu Isa Masiya.

Thambi zetu zinaondoshwa lini?
Katika ubatizo.

Katika majira gani tena?
Wakati wa kutubu.

Kutubu nini?
Kuzichukia na kuziacha thambi zetu.

XI.

Siri ya dini yetu, ndio nini?
Kitu kwa'nje kinachoonyesha neema iliopo kwa ndani.

Siri ngapi zimewapasa watu wote?
Mbili, siri ya Ubatizo, na siri ya Mwili na Damu ya Bwana.

Nana aliyeziamurn siri hizi?
Bwana wetu Isa Masiya.

Ameziamuru wapi?
Katika Kanisa.

Kwani ameziamuru?
Zituletee neema.

Neema ndio nini?
Msaada na upendeleo wa Muungu.

Siswi tunaweza kufanya neon jema pasipo neema?
Siyo, hatuwezi.

Tupateje neema?
Kwa kusali na kwa siri takatifu.

Kusali nini?
Kuinua roho kwa Muungu.

Neema za siri zimetoka wapi?
Zinatoka katika sadaka ya kufa kwake Bwana wetu Masiya.

XII.

Umebatizwa kwa kitu gani?
Kwa maji.

Umebatizwa kwa jina gani.
Kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.

Wakati wa kubatizwa umefanya nini?
Nimefanya maagano na Muungu.

Umefanya ahadi gani?
Kumchukia Shetani na kazi zake.

Kazi za Shetani nini?
Thambi zote na makosa yote.

Umefanya tena ahadi gani?
Kuiamini Imani masihiya.

Maana yake kuamini?
Kusadiki na kukubali.

Nione wapi walivyoviamini Wamasihiya?
Katika Imani zetu.

Umefanya tena ahadi gani?
Kuzishika amri zote za Muungu.

Muungu amekufanya nini?
Amenifanya kiungo cha Masiya.

Nini tena?
Mtoto wa Muungu.

Nini tena?
Mrithi ufalme wa mbinguni.

Neema halisi ya ubatizo nini?
Neema ya kuzaliwa kwa roho, na kutakasika kabisa.

Kuzaliwa kwa roho, maana yake?
Kupata uzima mpya na mtakatifu.

XIII.

Siri ya pili nini?
Siri ya Mwili na Damu ya Bwana.

Kwani ameiamuru Bwana wetu?
Itukumbushe kufa kwake.

Kwa maksudi gani tena?
Ituletee pato la kufa kwake.

Fungu kwa 'nje ya siri hii nini?
Mkate na divai.

Fugu kwa ndani nini?
Mwili na Damu yake Masiya.

Ni siri tu?
Ni tena sadaka masihiya.

Sadaka maana yake nini?
Kitu alichopewa Muungu.

Neema halisi ya siri hii nini?
Kupata chakula cha roho.

XIV.

Tutakapokwisha kufa tutakuwaje?
Miili yetu itakuwa vumbi.

Roho zetu zitakuwaje?
Zitangoja mwisho wa ulimwengu.

Kwa siku ya mwisho zitafanyaje?
Zitaungana na miili.

Kwani?
Tuamuliwe katika roho na mwili pamoja.

Vitu vinne vya mwisho vipi?
Kufa, Hukumu, Mbingu na Jehannum.

Imetupasa kuvifikiri vitu hivi?
Ndio, imetupasa kuvifikiri sana.

Imetupasa kufikiri nini tena?
Uzima na mauti ya Bwana wetu Isa Masiya.

Imetupasa kukumbuka sikuzote nini?
Ya kwamba Mwenyiezi Muungu anatuona.

Tumtumikieje?
Kwa Imani, kwa Matumaini, na kwa Mapenzi.

Vitendo vyetu pia vifanywewje?
Kwa sifa na heshima ya Muungu.

Utukufu uwe kwa BABA, na kwa Mwana,
na kwa ROHO Mtakatifu, ulivyokuwa
mwanzo, ulivyo sasa, uta-
kavyokuwa milele.

AMINA.


Project Canterbury